Mark 15:33-38

33 aIlipofika saa sita, giza liliifunika nchi yote hadi saa tisa. 34 bMnamo saa tisa, Isa akapaza sauti, akalia, “Eloi, Eloi, lama sabakthani?” Maana yake, “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?”

35Baadhi ya watu waliokuwa wamesimama karibu waliposikia hayo, wakasema, “Msikieni anamwita Ilya.”

36 cMtu mmoja akaenda mbio, akachovya sifongo kwenye siki, akaiweka kwenye mwanzi na akampa Isa ili anywe, akisema, “Basi mwacheni. Hebu tuone kama Ilya atakuja kumshusha kutoka hapo msalabani.”

37 dKisha Isa akatoa sauti kuu, akakata roho.

38 ePazia la Hekalu likachanika vipande viwili kuanzia juu hadi chini.
Copyright information for SwhKC